1. HAKIKISHA CHAKULA CHA KUKU WAKO KINA MCHANGANYIKO WA VITU HIVI VI 5
●MADINI👉 Kazi ya madini ambayo ni CALCIUM ni kuimarisha Mifupa, Mfumo wa fahamu, Uzazi, Kutengeneza ganda la yai na Inatumika kulisukuma yai na vyanzo vya CALCIUM ni Chokaa, Mifupa, Dcp na Dagaa.
●WANGA👉 Kazi ya wanga ni kutia nguvu mwili na vyanzo vya wanga ni Pumba za Mahindi, Ngano au Mtama.
●MAFUTA👉 Kazi ya mafuta ni kutia nguvu na joto mwilini vyanzo vya mafuta ni Mashudu ya alizeti, Pamba au Karanga.
●PROTINI👉 Kazi ya protini ni kujenga na kukarabati mwili na vyanzo vyake ni Damu iliyo kaushwa, Unga wa soya, Mchwa na Dagaa.
●VITAMIN👉 Kazi ya vitamin ni kuulinda mwili dhidi ya magonjwa kama vile kuvimba macho na mengineyo vyanzo vya. vitamin ni majani ya Mipapai na Mchicha.
2. WAPATE MASAA YA MWANGA YA KUTOSHA (LIGHTING)👇
Mwanga husisimua pituitary gland kwenye kuku ili kuchochea uzalishaji mwingi wa mayai, mtiririko mzuri wa utagaji wa mayai kuku huhitaji masaa 16 hadi 24 kwa mfano kuna baadhi ya majira ya mwaka ambapo jua huwahi kuzama na kuchelewa kuchomoza hivyo hu7bisha masaa ya mwanga kuwa machache kwa siku hivyo huathiri uzalishaji wa mayai kwa % kubwa ndy 7bu ya kuku wengi kuruka siku 1 au 2 yaani kutotaga kila siku.
SULUHISHO LA TATIZO LA KUPUNGUA KWA MASAA YA MWANGA👆
Unaweza kuwa wekea taa za umeme (ARTIFICIAL LIGHT) ndani ya banda lako la kuku na uziwashe baada ya giza tu kuingia kwa masaa mawili hadi ma 3 hii itaongeza utagaji wa kuku wako kwa 20% hadi 35% hii inaonyesha jinsi gani mwanga ni wa muhimu sana kwa kuku watagaji.
3. HAKIKISHA BANDA LAKO NI SAFI MUDA WOTE👇
Ili kusiwe na wadudu kama Utitiri, Chawa na Viroboto maana wadudu hawa huwasumbua sana kuku huwafanya wapunguze kutaga kwa % kubwa maana huwanyonya damu hivyo uwe unawanyunyuzia dawa ya akher powder ndani ya manyoya na banda mara kwa mara.
4. Wapatie maji ya kutosha na uwe unasafisha vyombo vya maji kila siku kwa sabuni ili kuzuia magonjwa nyemelezi yatokanayo na uchafu .
5. Wachunguze mara kwa mara kama wana dalili za kuumwa na endapo kama dalili zipo watibu mara 1.
6. Wawe na sehemu ya wazi ya kuzunguka zunguka na kuparua parua.
Note wakati mwingine inadhaniwa kuwa jogoo anaweza kufanya tetea atage mayai mengi hakuna kitu kama hicho kazi ya jogoo ni 1 tu kurutubisha tu mayai yaweze kutotolewa kama kuku wako anataga mayai machache ukaona umwongezee jogoo hata taga kabisa maana inatakiwa jogoo 1 kwa tetea 5.

0 Comments