*CHAKULA*

Kama ilivyo kwa viumbe wengine kuku nao wanahaki ya kupewa chakula bora na chakuwatosha kwa muda wote hii ni hakiyao kisheria ANIMAL WELFARE ACT.

 

Kwa kuzingatia hilo huu ni mwongozo wa ulishaji wa kuku wa *MAYAI, CHOTARA, WA KIENYEJI* NA aina nyingine zinazozalisha mayai

 

 *Layer starter mash wiki 1-8 au 1-7*

 

 *Layer grower mash 9-17 *hii inaenda mpaka kuku atakapo dondosha yai la kwanza*

 

 *Complete layer mash* kuanzia wiki ya 18 mpaka kuku atakapo acha kutaga au utakapo amua kumuuza.

 

NB kuku wanatakiwa walishwe kwa kiwango wanacho stahili kulingana na aina ya kuku na umri wa kuku wenyewe

 

 *KUKU WA NYAMA*

 

 *BROILER*

Hawa ni kuku ambao kwa asili wanao uwezo wa kukua na kujaza nyama mapema na huweza kufikia kilo 2 ndani ya siku 42 wakilishwa chakula chenye ubora

 

 *RATIBA YA ULISHAJI*

Broiler starter crumble siku 1-13

 

Broiler Grower pellets siku ya 14- 22

 

Broiler Finisher pellets siku ya 23-35

 

Hapo tunategemea utakua umeshauza kuku wote broiler bandani (japo wengine huuza broiler siku 28-32) kwa kutegemea uzito wa kuku.

 

 *CHOTARA KAMA KUKU WA NYAMA*

 

Broiler starter crumble siku 1-21

 

Broiler Grower pellets siku 22-41

 

Broiler finisher pellets siku 42-70...au kama utauza ndani ya miezi mitatu utakuwa ukiwapa finisher

 

NB usije ukachanganya kuwalisha sterter kuku wakubwa watapungukiwa baadhi ya viinilishe ...wala usiwalishe finisher kuku wadogo watapata matatizo kwenye ukuaji

 

PIA unapo hama kutoka chakula cha aina moja kwenda nyingine ni vema ukawa unawachanganyia ili wazoeechakula na wasipate stress zitakazopelekea kupungua kukua MFANO starter kwenda grower unaweza changanya siku ya 11-13 kisha unaanza kuwapa grower pekee Siku ya 14.

 

 *RATIBA ZA CHANJO*

 

Kuku wanaokaa muda mrefu kama Wa MAYAI, CHOTARA,  KIENYEJI

 

Siku ya 1 chanjo Marek's

Siku ya 7 chanjo ya Newcastle/kideli

Siku ya 14 chanjo ya gumboro

Siku ya 21 chanjo ya kideli/Newcastle

Siku ya 28 chanjo ya gumboro

Siku ya 30 chanjo ya ndui

Baada ya miezi mitatu dawa za minyoo

Rudia chanjo ya kideli kila baada ya miezi mitatu

 

 *KWA KUKU WA NYAMA/ BROILER*

 

Hawachanjwi mareks

Siku ya 7 chanjo ya Newcastle

Siku ya 14 chanjo ya gumboro

Siku ya 21 chanjo ya kideli

Wafugaji wengi wamekua wakichanja hivyo kwakua huuza kuku ndani ya siku 28-30

 

Kama utauza kuku baada ya siku 40 chanja chanjo ya gumboro siku ya 28.

 

 *Kumbuka*

Chanjo  zote zamaji zinatakiwa zikae ndani ya muda wa saa 1-2...baada ya hapo mwaga maji OSHA vyombo na badilisha maji ya kawaida

 

Zingatia usafi wa maji na vyombo kabla na baada ya chanjo

 

Kama utatumia maji ya mvua au usiyoamini kuwa ni masafi kwajili yachanjo yatibu kwa kidonge kinaitwa CEVAMUNE/Chlorex blue.

 

Nimependa tujifunze hayo kwa Leo nawatakia ufugaji mwema