Entrepreneurs Tanzania: UJASIRIAMALI---UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI

 

1. Safirisha chanjo yako kwenye kifaa ambacho kinatunza joto sawia muda wote na kifaa hicho huwa na vipande vya barafu .

NB; kuku wanatakiwa wapewe vitamin ( vitalyte au antstress yoyote) siku moja kabla ya chanjo na siku moja baada ya chanjo ili kusaidia kuondoa msongo (stress).

 

2. Usichanganye chanjo na vitamin.

 

3. Usichanje kuku wagonjwa.

 

4. Kama kuku wako ulikuwa unawapa antibiotic yoyote unatakiwa usitishe kuwapa siku mbili kabla ya chanjo na kisha utaruhusiwa kuwapa tena siku 2 baada ya kuwapa chanjo.

 

5. Kama chanjo unawapa kupitia maji ya kunywa hakikisha chanjo haikai kwa muda usiozidi masaa mawili ndani ya banda na kisha baada ya masaa hayo ondoa chanjo na osha vyombo vyako kwa maji safi na kisha wawekee maji safi na salama yasiyokuwa na mchanganyiko wowote .

 

6. Ili chanjo iweze kunyweka na kuku wote unatakiwa kuwanyima maji kuku wako kwa muda wa masaa 2-3 kisha baada ya hapo waweza kuwapatia chanjo.

 

7. Hairuhusiwi kutunza chanjo kwenye "freezer". Chanjo inatakiwa kuhifadhiwa kwenye joto la kati ya 2-8 degree centigrade.

 

8. Usitumie maji yenye chlorine wakati wa chanjo aidha tumia maji yaliyoondolewa chlorine.

9. Unashauriwa kutoa chanjo kwa kuku wako mapema asubuhi au jioni.

 

10. Wakati wa kuchanganya chanjo hakikisha unachanganya na 40% ya maji yote wanayokunywa kwa siku nzima. Kwa mfano huwa wanakunywa lita 20 kwa siku unatakiwa chanjo yako uichanganye na maji lita 8 ambayo yatanyweka kwa masaa 2.

 

11. Unaponunua chanjo hakikisha unasoma "expire date" na "batch number".

 

12. Hakikisha unapotoka kununua chanjo unakwenda moja kwa moja shambani na usizunguke nayo kwani inaweza kupoteza ubora kadri muda unavyozidi kwenda.

 

13.Hakikisha unamtafuta daktari hasahasa kwa chanjo zinazohusisha sindano ili achome sehemu inayohusika na kuepuka kukosea.

 

14. Zingatia maelekezo ya kila chanjo na USIJIONGEZE NA MAELEKEZO YAKO BINAFSI.

 

15. Izuie chanjo isipatwe na joto kali pamoja na mwanga mkali.

 

16. Hakikisha mabaki yote ya chanjo unayachoma moto na kuweka mbali na watoto.

 

FUGA KWA FAIDA