Kwanza kabisa hawa ni kuku ambao wengi walizoea kuwafahamu kwa jina la *KENBRO* (Kenya), ila kwa Tanzania tunaita *(TANBRO)* Kuku wazazi wanaitwa *REDBROW*

 

Kuku hawa wanarangi tofauti tifauti kutokana na rangi za jogoo wao, kuku wazazi wanarangi moja ( *Rangi nyekundu sio kama damu)*

 

Ila aina za jogoo zipo aina nne tofauti

 

👉 Wapo red (wekundu).

 

👉Wapo Black ( Kanga kanga).

 

👉Wapo nacked nakes ( Vishingo).

 

👉Wapo Tricolour ( rangi mchanganyiko).

 

 *Hivo basi ukinunua vifaranga aina ya Tanbro utakutana na hizo aina tofauti za vifaranga.*

 

Asili ya kuku hawa ni ufaransa ( *France* ) na sisi I?huagiza kuku wazazi ( Redbro kutoka huko ufaransa) wanasambazwa na kutengenezwa na Kampuni kubwa sana ya kuku duniani inayoitwa ( *HUBBARD* ).

 

 *SIFA ZAO KUJITOFAUTISHA NA WENGINE.*

👉Ukuaji wa haraka ( kuku hawa ukiwalisha starter bora hukua haraka kuliko aina nyingine za kuku na wanaweza kufikia mpaka kilo 4 ndani ya miezi minne - Mitano.

 

👉Viwango vidogo vya vifo ( chini ya uangalizi mzuri idadi ya vifo hasa wiki mbili za kwwaza huwa chini ya asilimia moja) na wakikua vifo huadimika kwa kiwango kikubwa.

 

👉Wanaumbo kubwa na lenye mvuto kibiashara( sokoni)

 

👉Wanaonekana kuwa kama kuku wa kienyeji kabisa

 

👉Wanaanza kutaga wafikapo wiki ya 19-21 na mayai huwa kati ya 180- 220  kwa wiki 81 kwa standard, ila inaweza kunda zaidi ya hapo kulingana na utakavo wabakiza bandani.

 

👉Jogoo wao ni bora sana hivo mayai ya kutotolesha huzalisha vifaranga kwa zaidi ya 95% ( mayai yanakua na mbegu).

 

👉Kuku hawa wanafugika kwa mifumo tofauti ( Nusu huria , Mfumo wa ndani na Mfumo wa huria)

👆Kitaalamu tunashauri wafugwa kwa Nusu huria au Kufugiwa ndani kwa mafanikio yaliyo tukuka.

 

👉Ni wastahimilivu wa magonjwa na wanaosikia dawa wakitibiwa.

 

👉 Kwa sababu ya tabia zao za ukienyeji wanaweza kufugika kwa zaidi ya miaka miwili

 

 *MIFUMO YA ULISHAJI*

 

Tanbro kama kuku wengine chotara mifumo ya ukishaji haitofautini, hivo unaweza kuwafuga kama wafugwavyo kuku chotara wengine.

 

👉Broiler Starter ( Wiki 2 za kwanza , kisha Layer starter mash wiki ya 3 hadi 7/8).

 

👉Grower Mash , wiki ya 7/9 mpaka pale kuku wanapo anza kutaga ( wiki 19-21).

 

👉Layers Mash pale watakapo anza kutaga mpaka utakapo amua kuwauza bandani.

 

👆Kuku hawa walishwe kwa chat za ulishaji kwa uzito na umri kama aina nyingine za kuku kupata matokeo bora.

 

 *RATIBA YA MWANGA*

 

Kwakua tunatarajia matokeo bora kabisa kutoka kwa kuku wetu hivo nimeona vema nikueleze ratiba za mwanga hasa kwa kuku wanao karibia kuanza kutaga.

 

Kuanzia wiki ya 16 wape masaa 14 ya mwanga

 

Wiki ya 17 masaa 15 ya nwanga

 

 *Wiki ya 18 wape masaa 16 ya mwanga na endelea kuwapa hivo baada ya kuanza kutaga na kuendelea*

 

RATIBA ZA CHANJO

 

 *Kama inabozingatiwa kwa kuku wengine hawa pia wanatakiwa kuchanjwa kwa kufuata ratiba stahiki.*

 

👉Siku 1 chanjo ya mareks ( hatchary) na Ib + ND spray.

 

👉Siku ya 7 na 21chanjo newcastle( kideri) rudia kila baada ya miezi mitatu.

 

👉Siku ya 14 na 28 chanjo ya Gumboro (IBD Vaccine).

 

👉Siku ya 30 chanjo ya ndui( maeneo yanayo wahi kupata ndui tumekua tukichanja mapema wiki ya 3, chanjo ya bawa).

 

 

 *Dawa za minyoo*

 

👉Wapewe pindi wanapo fika miezi miwili kisha kila baada ya miezi mitatu  NB Hakikisha wanapo fika umri wa wiki ya 19-20 wamepewa dawa za minyoo kuwaandaa watage bila kusumbuliwa na minyoo.