ULINZI WA VIUMBE HAI /KUKU DHIDI YA MAGONJWA

Magonjwa ya kuku imekua fimbo kubwa sana kwa mfugaji hali inayopelekea kuongezeka kwa garama za kununua madawa....vifo vya kuku kuongezeka...kuku kupoteza uzito na thamani katika soko....kuteketea kwa mitaji ya wafugaji na hata kukata tamaa ya kuendelea kufuga.

Kwa kutambua hilo yafuatayo unaweza kuyatumia yakakusaidia kwa kiasi kikubwa sana kupunguza magonjwa ya kuku bandani

Moja hakikisha mradi wa kuku unakua na usimamizi mzuri muda wote kutoka kwa mtunzanzi wa kuku hasa kuwaangalia kuku wako Mara kwa Mara na kubaini changamoto zao

Mbili hakikisha banda lako limejengwa katika ubora unaostahili kwa kuzingatia uwepo wa wavu nusu ukuta na tofali au material yoyote ya kujengea nusu ukuta 0.5-0.7 m

Tatu hakikisha umejiwekea sheria za kuzifuata kwaajili ya kuwalinda kuku wako...mfano kuwepo mabuti ya kuingia nayo bandani pekee...ziwepo nguo maalumu za kuingia nazo bandani...vifaa vya kuku visihamishwe kutoka banda moja kwenda jingine......

Mhudumu wa kuku anapaswa kuanza kuwahudumia kuku wadogo kwanza ndipo aende kuwahudumia kuku wakubwa

Usifuge kuku kwa kuchanganya na ndege wengine kama BATA ,KANGA , NJIWA

Hakikisha mfumo wako wa ulishaji na unyweshaji kuku ni mzuri unao muwezesha kuku kupata maji masafi muda wrote

Hakikisha kuna dawa za kuulia wadudu mlangoni za kukanyaga kama FARM GUARD kuua vimelea pindi utokapo na unapoingia bandani

Banda la kuku linapaswa kusafishwa kwa dawa za kuua wadudu kama V-RID au TH4..nakupumzishwa kwa muda usiopungua siku 14 kisha uingize kuku wengine

Kuku wanatakiwa kupewa kinga za magonjwa yote ya virusi ili kuwafanya wawe na kings imara ya magonjwa

Epuka kuchanganya chakula cha kuku kwa kutumia pumba zilizo vunda au dagaa waliovunda,,utapunguza magonjwa

Zuia uwezavyo watu wasio na ulazima kuingia bandani...mfano watu kuja kuwatazama kuku wako mara kwa Mara...kila mnunuzi kumwingiza bandani kuangalia kuku kila wakati hupelekea magonjwa kutoka shamba moja kwenda jingine

Pale uonapo dalili ya kuku kuumwa watenge...kisha utafute usaidizi wa madaktari kugundua ni ugonjwa upi unawapata kuku na uwape Tiba kwa kumaliza dozi....usipendelee kubadilisha dawa za kuku kablaa dozi haijaisha huwapa usugu wa kupambana na magonjwa

Kama unashamba kubwa magari...au pikipiki zinazoingia kwenye shamba zipuliziwe dawa za kuua vimelea wa magonjwa

Hakikisha banda lako linakua kavu muda wote hii itapunguza saana magonjwa kama coccidiosis ambayo husumbua na kuua kuku wengi kwa wafugaji..

Kwa vifaranga hakikisha wanapata joto lakutosha wiki 2 za kwanza....pia wapewe chakula chenye ubora unaotakiwa

Mabanda yako yajengwe kitaalamu kufuata uelekeo wa upepo...pia kuangalia JUA...EAST -WEST...direction

Hakikisha vyomba utakavyo kua ukivitumia ni visafi na maji utakayo kua ukiyatumia ni salama kwa matumizi ya kuku

HIZO NI BAADHI TU YA TARATIBU ZA MUHIMU KWAAJILI YA KUZUIA MAGONJWA KWA KUKU

Imeandaliwa na GREYSON KAHISE mtaalamu wa kuku

Simu 0769799728/0653387629