FOWL POX DISEASE/NDUI

Huu ni miongoni mwa magonjwa ya virusi ambayo yamekua yakishambulia kuku kwa aslilimia kubwa.

 Chanzo
👉Ugonjwa huu husababishwa na virusi, Fowl Pox Virus

Virusi hawa huwapata kuku wa rika zote, wakubwa na wadogo

👇Kusambaa

👉Ugonjwa huu husambaa haraka sana kwenye mazingira au banda Mara baada ya kuingia

👉Kwa maeneo mengine , yenye mbu wengi inasemekana kwamba piaa huenezwa na mbu.

👆 Ugonjwa huu pia hufichwa au kubebwa na ndege wengine hasa bata na kupeleka kwa kuku.

 ðŸ‘‡Tiba
👉Ugonjwa wa ndui ya kuku hauna tiba.

Badala yake ni muhimu kuchanja kuku wawapo na umri wa siku 30 au wiki (4-5).

👆Nini ufanye iwapo kuku wako wameshapata ndui.
👉Kuku mwenye ndui, huonesha vinundu/vipele kwenye maeneo yaliyo wazi hasa mdomoni, machoni na mwilini.

👉Baadhi yao huvimba macho na wakati mwingine kupata vidonda

👇Kuku akifikia kiwango hicho  fanya haya
👉Mtenge kundini
👉Msafishe vidonda kwa maji ya chumvi
👉Kama atatoa damu, mpake iodine
👉Mpe ant biotic OTC 20% au 50%(wote bandani)
👉Hakikisha amepona kabisa
👉Baada ya angalau wiki 1-2 tangu kupewa dawa wachanjwe

JINSI YA KUCHANJA
👉Wasiliana na daktari alie karibu na wewe mahali ulipo akusaidie kwa hili zoezi.

Kama umeshindwa kupata huduma hiyo

👉Nunua chanjo ya ndui
👉Changanya chanjo na maji yake

👇Mimina maji ya kuyeyushia chanjo ndani ya chupa yenye kidonge cha chanjo

👉Chukua sindano na kuanza kuchanja kuku wako eneo la bawa( lisilo na mfupa) Wing web.

👉Ukimaliza kuchanja na chanjo ikawa imebaki
, usiihifadhi teketeza au kutupa masalia hayo.

Angalia picha hapo juu kuona sehemu ya kuchanja kuku wako. 👆👆

Imeandaliwa na
👇👉Greyson Kahise
👉👉Mtaalamu wa kuku
 ðŸ‘‰ðŸ‘‰0769799718 0715894582

Pata kitabu changu cha ufugaji kuku kitakufaa sana 10000 mikoa yote TZ.