ZINGATIA YAFUATAYO PINDI UTUMIAPO FORMULA YOYOTE YA KUCHANGANYIA CHAKULA.

Kama ifahamikavyo chakula huchukua karibu 75% ya gharama ya uzalishaji kwa kuku, hivyo wafugaji wengi wamekua wakikimbilia kupata formula ya kuchanganyia chakula.

Yafuatayo yazingatiwe
👉Pata formula ya chakula sahihi, kwa mtu mzoefu( mfugaji), mzalishaji wa chakula, wataalamu, au formula iliyo thibitishwa ubora wake practically ( usigoogle formula ukaanza kulisha kuku wako ).

👉Chagua material/ malighafi za kuchanganyia chakula, safi na kavu zisizo na uvundo.

👉Simamia upimaji wa malighafi muda na wakati wa kuchanganyiwa mfn: Unaweza kwenda mashineni ukasema uwekewe soya kg 20 ukawekewa kg 15 bila kujua, hii itaathiri moja kwa moja ubora wa Formula uwe makini.

👉Usifanye marekebisho ya Formula uliyopewa bila kuwasialiana na mtu aliekupa formula, Mabadiliko yoyote yanaharibu ubora wa formula kulingana na viwango alivyo kuwa ameweka mtengenezaji wa formula mfn: Umeambiwa uweke Premix nusu kilo wewe ukaweka robo kilo.


👉Epuka kubadilisha formula za chakula kwa kuku hao hao Mara kwa Mara

👉Simamia na hakikisha ulishaji wa kuku unafanyika kwa usahihi kulingana na maelekezo ya aliekupatia formula au chakula.

👉Pindi uonapo uzalishaji wa kuku haukupi matokeo kwa wakati wasiliana na aliekupa formula mapema, ili kama kuna marekebisho yafanyike kabla kuku hawajafikia umri mkubwa

👉Hakikisha unafuata ratiba au muda sahihi wa mwanga kwa kuku

Karibu upate
FORMULA YA LAYERS, CHATARA 20000

na KITABU CHA FUGA KUKU KITAALAMU 10000

👇Imeandaliwa na
 ðŸ‘‰Greyson Kahise
👈Mtaalamu wa kuku
 ðŸ‘†0769799728 0715894582