*Sehemu ya kwanza*

Chakula cha kuku ni mchanganyiko wa viini lishe mbalimbali na kiini lishe lazima kiwe kwenye kiwango sahihi kulingana na umri wa kuku.
Viini lishe anavyohitaji kuku:-
~wanga
~protini
~madini
~mafuta
~Vitamini
~maji

Mchanganyiko sahihi wa viini lishe humwezesha kuku kukua upesi.
Viini lishe nilivyovitaja hapo juu hupatikana katika aina mbalimbali za viungo vya chakula cha kuku kama ifuatavyo:-

*Wanga*
 -hupatikana katika pumba ,chenga au dona ya nafaka kama mahindi au mtama aina ya serena,lulu nk

*Mafuta*
-hupatikana katika karanga au alizeti au ufuta mbegu hizi zikikamuliwa mbegu hubaki na kiasi cha mafuta .

*Protini*
-hupatikana katika mashudu ya alizeti,pamba,dagaa, damu ya wanyama kama ngombe ,mbuzi nk
..pia katika unga wa mbegu za jamii ya kunde kama maharage,kunde ,soya nk

*Madini*
-madini makuu hapa ni calcium na phosphorus pia sodiam na chlorini haya hupatikana katika unga wa mifupa ya wanyama iliyochomwa,chokaa maalumu ya mifugo,chumvi na hata majivu ya kawaida ya jikoni.

*Vitamini*
-hupatikana katika majani mabichi kama lusina,majani ya mpapai,mchicha, chainizi, nk
...waweza kukausha majani haya  kivulini na kutwanga upate unga wake uchanganye kwenye chakula .

*Maji*
-maji safi na salama ni mahitaji makuu ya kuku.
bila mahitaji haya hapo juu kuku huweza kupata matege,hutaga mayai ganda laini kutokana na kukosa madini.kitaalamu madini tunaweza kuyaongeza kwa kutumia Premix na DCP kwa kiwango sitahiki.
Kuku akikosa vitamini hupata upofu wa macho.
Japo kua damu ina protini kwa wingi tumia ukiwa na uhakika wa kuipata muda wote maana ukiikosa kwenye mchanganyiko wako ni mwanzo wa kuku wako kudonoana.

Mwisho wa sehemu ya kwanza na sehemu ya pili itakuwa ni kanuni za cha mchanganyiko wa vyakula kwa rika mbali mbali za kuku