🐓Sifa ya Yai Lenye sifa ya kutotolewa.

1. Hakikisha kuku wamepandwa vizuri na jogoo na hii ni Kwa kuzimgatia uwiano (ratio) nzuri ya majike na Majogoo.

2. Zingatia Yai Lisiwe na Nyufa au michirizi ya damu.

3. Zingatia Yai Lisiwe na uchafu wa choo Cha kuku.

4. Yai Lisishikwe na mikono yenye maji maji Wala lisioshwe.

5. Yai Lisiwe limezidi siku 14 tangu kutagwa.

🐓Namna ya kuhifadhi yai ili Liwe na ubora na liweze kuanguliwa ni:-

Hifadhi mayai yako sehem yenye hewa nzuri, au katika chumba chenye hewa ya kawaida (normal temperature).

Hifadhi yai katika trey za mayai na elekeza ncha iliyochongoka iwe chini Ili lipate hewA ya kutosha Kwa kijusi ndani ya Yai na sehemu bapa au mduara wa kawaida ikielekea juu.

*#kuku ni mali*