1.Hakikisha banda lako liko safi wakati wote na kuweka matandiko yakutosha walau inch 1-2.
2.Hakikisha unapulizia dawa zenye ubora kuondoa vimelea vya magonjwa wakati wote.
3.Hakikisha unachovya miguu au kubadili viatu kila unapoingia na kutoka bandani.
4.Hakikisha unasafisha vizuri vyombo vya chakula na maji.
5.Hakikisha unachanzo kizuri,cha uhakika na salama kwa ajili ya kuleta nishati ya joto bandani hasa kwa vifaranga na kipindi cha baridi kali inapobidi.
7.Hakikisha unachukua vifaranga bora wakati wote.
8.Hakikisha afya njema kwa mifugo wako wakati wote hasa kwa kujifunza tabia zao za kawaida wanapokua na afya njema na mazingira ya usalama ukitofautisha na wakati wanapokuwa wagonjwa.
9.Hakikisha wanapata hewa safi, maji safi,chakula safi na salama wakati wote.
10.Hakikisha unawapatia virutubisho vya ziada wakati wote inapohitajika kulingana na mahitaji ya mifugo yako.

KUMBUKA: Banda bora ni Muhimu sana kwa mfugaji yeyote mwenye nia dhabiti ya kufanya ufugaji wenye tija