Usibadilishe chakula cha kuku kutoka aina moja, kwenda aina nyingine ghafla.

Mfano, vifaranga vikifika miezi miwili, usiwape leo Starter na kesho ukawapa Growers.
Miili yao itashituka, na wanaweza kupunguza ukuaji.

Mfumo mzuri wa kuwahamisha kuku wako toka chakula aina moja kwenda kingine ni:

Siku 1 - Wiki 6 = Starter.
Wiki 6 - Wiki 8 = Changanya nusu Starter na nusu Growers.
Wiki 8 - Wiki 18 = Growers.
Wiki 18 - Wiki 20 = Changanya nusu Growers na nusu Layers.in
Wiki 20 na kuendelea = Layers.

Muhimu:
Formula za chakula cha Growers na Layers hutofautiana kulingana na aina ya kuku, mfano Kienyeji, chotara au kisasa.