Limeandaliwa na 
 *Greyson Kahise* 
Mtaalamu wa kuku
0769799728
 *0715894582*

👉Nimekua nikiulizwa maswali mengi Sana juu ya nini kinahitajika ili kufanikiwa kufuga kuku wa nyama, Hapa nitaainisha baadhi muhimu Tu.

👆 *Moja* *BANDA BORA*, Banda linaweza kutofautiana Ujenzi wake kutokana na ukanda ( Joto au Baridi), Banda liwe na sehemu ya Sakafu, Tofali au Bati au Mbao kwenye ukuta kutoka kwenye msingi, Wavu kupanda juu Hadi kwenye Lenta ( *Banda Bora liwe na nyavu pande mbili ndegu Mashariki na magharibi ) kuruhusu hewa kuingia na kutoka.* Kitaalamu *BROILER 10* WAKAE KWENYE *MITA MRABA MOJA*  Mfn kuku 500 wakae kwenye Banda la Ukubwa WA Mita mraba hamsini *unaweza Jenga Upana Mita 5 urefu mita 10*.

👆 *MAHITAJI WAKATI WA KUWEKA VIFARANGA*
👉 Vifaranga Bora ( Kutoka Kampuni ya uhakika).
👉Chakula Bora ( Kutoka Kwa wazalishaji wa uhakika).
👉Vyanzo vya uhakika vya joto ( *Inategemea wingi wa Vifaranga chagua kitakacho FAA, ama Vyungu, au Majiko ya mkaa, ama Taa za joto, ama Brooder za gesi ama Brooder za umeme Angalia urahisi mahali ulipo).*
👉Maranda Bora na masafi ( Ya Mbao au Mpunga) yaandaliwe walau wiki moja kabla ya kuleta vifaranga.
👉 *Maturubai* na *Plywood* kwajili ya kutengeneza sehemu ya kulelea vifaranga.

 *VYOMBO VYA MAJI NA CHAKULA*
👆Kitaalamu vyombo vya maji na chakula inapaswa viwepo bandani wakati unapuliza dawa ili navyo vipuliziwe dawa( *Usinunue Kwa Dharula).*
👉Vyombo vimetofautiana Ukubwa na Mzunguko , Idadi ya vyombo inategemea Ukubwa WA vyombo unavyotaka kutumia.
👆Kwa vifaranga tunashauri uanze na Sahani ( *Panfeeder au Brown paper* ) hizi hushawishi vifaranga Kula na kufikia uzito WA siku ya 7 mapema.
🐓 *Kwa wastani Drinker* moja Kubwa ya kipenyo cha 40cm  ihudumie kuku *60-80* , mfn Belly  Drinker 

🐓Drinker ndogo ya kipenyo cha 35cm ihudumie kuku 30-35, Drinker ndogo ya Lita 3  kuku 20-25.

👉 *Feeder kubwa* Zenye kipenyo  cha *40 cm* ihudumie kuku 30 na *feeder ndogo zenye kipenyo cha 30 cm zihudumie kuku 20-25*

NB: VYombo hivi vipangwe kwenye mistari vya maji pekeake na Chakula pekeake ( *Iwe Maji-chakula-maji-chakula-maji).*
‼️Muda WA kulea vifaranga unatifautiana , Msimu WA joto Kali maeneo ya joto wiki moja, Ila misimu ya Baridi *Hadi wiki 2 au 3* kwenye kanda za baridi Kali.

👆 *MPANGILIO WA CHAKULA* 
🐣Hii inategemea Kampuni unayotumia kulisha Ila Broilers 
🦅STARTER CRUMBLE/PELLETS SIKU 1-14
🦅 GROWER PELLETS SIKU 15-22
🦅FINISHER PELLETS SIKU 23 HADI KUUZA.

 *RATIBA ZA CHANJO*
👉Hiki ni kipengele Bora na cha lazima kukitekeleza sio Kwa kupenda ni Muhimu 
👆 Newcastle siku ya 7
👆Gumboro siku ya 14
👆Gumboro siku ya 14
 *Ama*
👉 Newcastle siku ya 7
👉 Gumboro siku ya ya 14
👉 Newcastle siku ya 21

 *IKIWA KUKU WAKO WATAKAA ZAIDI YA SIKU 28 itabidi uchanje Gumboro ya Pili.*

👉 *VITAMINS* & *VIRUTUBISHO* VINGINE.
👆Kwanza ifahamike wazi kwamba kuku wetu ili wakue vema na wawe na afya madhubuti wanahitaji Vitamin kama nyongeza ya virutubisho VINAVYO pungua kwenye chakula
‼️ *HATUSHAURI BOOSTER KUANZA KUTUMIKA MAPEMA WALAU BAADA YA SIKU 14 hapa mwanzo wapewe vitamin Tu.‼️*

🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓
👉Siku 1-5 *Multivitamin* au Vitamins plain *mfn* . Amintoto, Introvit A etc

‼️ *NB:Inawezekana kufuga bila dawa iwapo Mazingira yote yatawekwa vizuri. Antibiotics za mapema zinaua vimelea kinga na kumfanya kuku awe dhaifu.‼️* 


👉Siku 8-12 Vitamin plain( Vitamins zisizo na dawa yoyote). Mfn Amintoto, Introvit A+, Aminogrow, Galvet, Biospark etc.

👉Siku 15-19 ( Vitamins au Booster nzuri

👉Siku 22-kuuza ( Vitamin au Booster nzuri).

‼️ *SIO SHERIA KUTUMIA BOOSTER KAMA UNACHAKULA BORA UNAWEZA TUMIA VITAMINS PEKEE* ‼️

☝️Randa zibadilishwe au kugeuzwa pale zinapopata unyevu kuepusha Mrundikano WA amonia utakao leta mafua na shida zingine za Magonjwa kama Coccidiosis 

0715894582
Greyson Kahise