👉Kwanza Kabisa ifahamike chanjo Kwa kuku sio Chaguo ni Lazima Kwa usalama wa KUKU wako

👉Pia kuchanja kuku sio Kwa vile unavojiskia Ila Kwa Ratiba maalumu inayowekwa kutokana na umri wa kuku

 *HATUA ZA KUFUATA ZA KUTUMIA CHANJO IPASAVYO*

👉Nunua chanjo, kama inahitaji ubaridi hakikisha umefungiwa kwenye kifungashio Chenye barafu.

👉Safisha vyombo vya maji vya kuweka chanjo yako na ikifaa viache vikauke.

👉Kwa maji ya BOMBA, KISIMA NA MVUA, inashauriwa yachemshwe na uyaache yapoe kabisa ndipo utachanganya na chanjo.

👉Iwapo UTATUMIA vidonge vya kutibu maji MFN CEVAMUNE, CHLOREX BLUE, VACC-SURE nk. Utatakiwa kuloweka kidonge kwenye maji yasiyo na chanjo na changanya vizuri Kwa kifaa cha plastic,

👆Acha maji hayo yakae Kwa dakika 15-30 kisha changanya na chanjo yako.

👉Kama utatumia maziwa SKIMMED MILK weka grap 2 Kwa Lita moja ya Maji changanya vema na uache Kwa dakika 30.

 *UFUNGUZI WA CHANJO*
👉Kwa chanjo za Kuchanganya kwenye maji, Utakiondoa kichupa Chenye chanjo kwenye barafu yako au Friji
👆Utatakiwa kufungua chupa hiyo yenye kidonge cha chanjo ikiwa ndani ya Maji ambayo umesha yaandaa Kwa Kuchanganya chanjo yako.
👆Ukigungua koroga maji vema kuhakikisha chanjo imeenea kwenye maji
👆Wape kuku wako wanywe Kwa Muda WA masaa mawili.
👆Ondoa maji ya
chanjo na uoshe vyombo vyako, kisha weka maji ya kawaida kuku waendelee kunywa.

 *KWA CHANJO YA NDUI*
👆Fungua chupa yenye maji ya Kuchanganya kwenye kidonge

👆Kisha Fungua chupa yenye kidonge

👆Kisha mimina maji ya Kuchanganyia kwenye kidonge cha chanjo na utikise kilainike 

👆Anza kuchanja kuku wako

Nimejaribu kutoa machache Kati ya mengi yanayotakiwa kufuatwa kufanya chanjo KIUSAHIHI