Andaa banda lako liwe safi na lililo puliziwa dawa ya kuuwa wadudu na bacteria mfano V-rid au TH4 zoezo hili lifanyike mapema week 2 kabla ya kuleta vifaranga mlangoni weka maji ya kukanyaga yenye dawa ya farm guard
Andaa sehemu ya kulelea vifaranga/blooder unaweza tengeneza kwa singbod au mabox kwa kuweka mzunguko kimo kiwe 30cm au 40 cm
Weka randa safi kwenye blooder kimo kiwe 5cm ujazo wa landa
Tandika mifuko au magazeti juu ya randa hi itasaidia vifaranga kutambua chakula mapem
Masaa mawili kabla ya kuweka vifanga
Weka chakula na maji kwenye blooder hapa utatumia drinker na sahani au mfuko sambaza starter
Weka chanzo Cha joto kwaajili ya vifaranga unaweza tumia chungu Cha joto au taa ya umeme watt 200
Kwenye drinker weka maji yaliochanganywe na glucose pamoja na neoxychick inategemea na umbali vifaranga
Kwa siku ya Kwanza hadi ya tano maji ya kunywa vifaranga changanya na vitamin
Siku ya sita maji matupu
Siku ya saba wape chanjo ya kideli (Newcastle vaccine)
Siku ya 8 hadi ya 12 maji changanya na vitamin
Siku ya 13 maji matupu
Siku ya 14 wape chanjo ya gumbolo vaccine)
Siku ya 15 hadi 19 maji yenye vitamin
Siku ya 20 maji matupu
Siku ya 21 chanjo ya marudio utachagua Kati ya Newcastle vaccine au gumbolo
Siku ya 22 hadi 26 maji yenye vitamin
Siku ya 27 maji matupu
Siku ya 28
chanjo ya marudio kama siku ya 21 ulichanja gumbolo Basi leo utarudia Newcastle na kinyume chake
Week ya tano chanjo ya ndui
Week ya nane dawa za minyoo
Kumbuka muda wote huo hadi week ya nane chakula kinachotumika ni starter na utatakiwa kurudia chanjo ya kideli na dawa za minyoo Kila baada ya miezi mitatu
0 Comments