Ugonjwa huu huathiri kuku katika umri wowote na unapoingia kwenye kundi la kuku huweza kuua idadi kubwa ya kuku hao hadi kufikia 90%. Ndege wakubwa hustahimili kidogo kuliko wale wadogo kwasababu ya usugu mwilini (KINGA) uliojengeka kwa muda mrefu zaidi
 
Ugonjwa huu husababishwa na kimelea cha kirusi kiitwacho Avian paramyxovirus-1  na huenezwa kwa njia ya hewa na kugusana, kutokuwepo kwa usalama wa viumbe hai (biosecurity) katika shamba lako, uchafu unaoletwa na magari, viatu, vifaa vya kazi, ndege wa porini na watalii

DALILI ZAKE

Vifo vya ghafla muda mwingine  bila hata kuonesha dalili

Kuvimba shingo na kichwa

Kupooza (paralysis) kwa mbawa na miguu
 
Ute hutoka mdomoni na puani

Kuku walioathirika hupata kizunguzungu

Kuharisha uharo wa kijani

Kuzubaa, kusinzia na mabawa kushuka

Kuzunguka kama vile ana kifafa

Utagaji hushuka na mayai kuwa na  umbo lisilokuwa la kawaida

Zaidi ya  90% ya kuku huweza kufa

Kuku hufa  kwa kupinda shingo

TIBA

Ugonjwa huu hauna dawa zaidi ya chanjo tu lakini unaweza kutumia TRIMAZINE 30% pamoja na Vitamini kwa kuku walioathirika

KINGA

Ugonjwa huu ukitokea jitahidi kuwatenga kuku wagonjwa na kuku wazima

Zuia muingiliano wa kutoka banda moja kwenda banda lingine pia weka maji yenye dawa (Farmguard) mlangoni kabla ya kuingia bandani na hakikisha unakanyaga hayo maji yenye dawa

Kideri kinauzuiwa kwa njia  ya chanjo inayoitwa LASOTA.
 Chanja kuku wako kila baada ya miezi mitatu na mara nne kwa mwaka. (Fuata mtiririko sahihi wa chanjo ya  kideri)

Epuka kuingiza kuku wageni kutoka shamba usilolifahamamu na usilojua kuhusu historia ya chanjo