Wafugaji wengi wamekuwa wakipata hasara kutokana na utotoleshaji mbovu wa mayai kwani mengi huharibika bure. Hayo hutokana na kutozingatia maelekezo ya sifa za mayai bora yanayofaa kuatamiwa na kiatamishi.
Kabla ya kuweka mayai ndani ya kiatamishi hakikisha mambo yafuatayo yamezingatiwa kikamilifu;
Yai lisizidi siku 7 mpaka 10 tangu litagwe. Hii iina maana kwamba mayai yanayotakiwa kuwekwa kwenye droo ya kiatamishi lazima yawe ni yale ambayo hayajazidi siku 7 au 10 tangu yatagwe na kuku. Hivyo hakikisha suala hili wakati wa ukusanyaji wa mayai yaliyotagwa. Hivyo kama umekusanya mayai muda wa siku 10 mfululizo basi hutakiwi kuongeza tena yai jingine kwakuwa ile siku ya kumi (10) kumbuka tayari kuna mayai ya mwanzo kukusanywa yatakuwa tayari yameshakaa siku 10. Kwahiyo kama utaendelea kukusanya siku zaidi ya 11 basi yai la mwanzo kukusanywa lazima litolewe!
Mayai yahifadhiwe kwenye trei yakitoka kuokotwa bandani.
Zingatia uwiano mzuri wa majogoo kwa matetea (1:8-10)
Mayai ya mtago wa kwanza sio mazuri kwa kutotolesha. Hii ina maana kwamba kama kuku ameanza kutaga leo basi usichukue yai la leo bali anza kuokota yai la siku inayofuata, yaani yai la kwanza sio sahihi kwakuwa huenda likawa halijarutubishwa vizuri.
Mayai ya kuku mzee sio mazuri kwa kutotolesha
Kuku watagaji wanapaswa kupewa chakula bora na cha kutosha
Mayai yahifadhiwe sehemu isio na joto kali
Mayai machafu au yenye madoa ya damu hayafai kwa kutotolesha
Mayai yenye kreki (nyufa) hayafai kwa kutotolesha
Mayai yenye umbo kubwa sana au madogo sana hayafai kwa kutotolesha (yanatakiwa yawe na ukubwa wa wastani).
Mayai yenye viini viwili hayafai kwa kutotolesha
Yai lisihifadhiwe kwenye frigi (hifadhi sehemu yenye hewa ya kutosha na isio na joto kali.)
Mayai yahifadhiwe kwenye matrey.
Wakati unahifadhi mayai katika trei hakikisha sehemu ya yai iliyochongoka inaangalia chini
Tengeneza viota vya kutagia ili kuepusha mayai yasichafuke kuku anapotaga!wala yasiguse maji au kupasukiana
0 Comments