WAZO LANGU SIKU ZA USONI

INASIKISHA!INAHUZUNISHA!!KUONA

Makampuni yanashusha bei za vifaranga,,,vyakula vinapanda bei,,,lakini kuku wanashuka bei bandani na sokoni kila siku,,,,wakati mlaji wa mwisho amekua akiuziwa kuku kwa bei ileilee ya tangu zamani wafugaji tunaumia sana

MAONO NA MTAZAMO NI KUWA NA UMOJA KAMA WAFUGAJI KUKU KILA MKOA

Naamini kila mkoa kuna umoja wa wafugaji wa kuku au kama hakuna umoja wa kila mikoa kupitia groups hizi za kuku nitajitahidi kushawishi kwa kadri nitakavo weza umoja uundwe

Kilaa mkoa wafugaji wa kuku tujuane..tuwe na uongozi...tuwe tunafanya makubaliano hasa ya masoko kutokana na mabadiliko ya bei ya vyakula na vifaranga

Badaa ya muda nitaandaa links ambazo wafugaji wa mkoa husika watakua wakijoin na kuwasambazia wenzao kisha huko watapatikana wa kuzisimamia izo groups hatimae tuwe kitu kimoja kila Mkoa

Hii itasaidia saana huko mbeleni hata kuwa na sauti kwenye soko...kwa kujiwekea msimamo wa uuzaji wa kuku

Tukumbuke wanunuzi wa kuku huja bandani na bei zao wakijua wafugaji nilazima tuuze kwasababu kuku wakibaki bandani tutapata hasara

Ilaa huko mbeleni kama tutafanikiwa kuwa na msemaji wa kilaa mkoa na makubaliano ya kila mkoa itatufanya tuwe huru na msimamo hatimae KUKU WATUPE FAIDA

Nafahamu mwanzo wa kulianzisha hili ni mgumu ilaa mpaka sasa nimeanza kwa sehemu na mwitikio ni mkubwa sana

KARIBU TUUNGANE TUUPINGE HUU UKANDAMIZWAJI WA WAFUGAJI WADOGO

Greyson kahise  0769799728/0653387629

KUKU TAIFA KUBWA TUKIUNGANA TUNAWEZA TUUNGANE