MAANDALIZI YA SEHEMU YA KULELE VIFARANGA/ BROODING AREA

👆Brooder ( kinengunengu), hii ni sehemu ya muhimu sana , na yakuzingatia sana wakati wa malezi ya vifaranga

 SIFA ZA BROODER
👉Joto lakutosha
👉Randa/matandazo
👉Maji
👉Chakula
👉Hewa ya kutosha
👉Mwanga
👉Nafasi ya sahihi ya kutosha

👉👇nini sasa ufanye kuandaa brooder/ sehemu ya kulelea vifaranga.

👉Kwanza angalia idadi ya vifaranga wako,
👈Brooder inaweza kuwa ya duara, kama utalea vifaranga wachache

👈Kama utalea vifaranga wengi unaweza kutengeneza brooder ya pembe nne kwa kuzingatia vipimo.

MATENGENEZO YA BROODER YA DUARA

👉Tafuta siling board, ikate kwa urefu vipande vitatu (standard 30-40 cm) kimo, au wengine hukata Mara mbili *(katikati)*

👉Unganisha vipande ulivyo vikata kutengeneza duara lako, Mimi huunganisha kwa kuchana kibao kwa msumeno kitakacho shikilia siling board upande wa juu kwenye maungio.

👉Kitaalamu mita moja mraba hutosha vifaranga 40, ila eneo utakua unalitanua kwa kadri vifaranga watakavo kua wanaongezeka kukua.

👉Baada ya kutengeneza brooder yako, Weka randa za mbao au pumba ya mpunga ( walau wiki 1 kabla ya kuleta vifaranga)

👈Tandika gazeti, au mifuko, au Ground paper.

👉Wakati vifaranga wanakaribia  masaa  kadhaa kabla vifaranga kufika weka chanzo cha joto ( vyungu, Bulb, Gas heater). Kama chumba nikikubwa sana na joto litachelewa kushika kwenye sakafu washa masaa 24 kabla ya vifaranga kufika, Joto la sakafu, randa , na maji vinatakiwa vifikie joto la chumba.

👉Ingiza vifaranga wako, tayari wakute chakula  na maji bandani,

👉Hakikisha vifaranga wanapata chakula na maji muda wote ili wakue kwa uwiano, hasa wiki 2 za kwanza , ukikosea tu watapishana ukuaji

👉Vifaranga waanze kwa chakula cha Starter kwa wiki 6-8 za kwanza kwa kutegemea maelekezo ya chakula unacho tumia.

WENYE VIFARANGA WENGI
👉Andaa chumba chakulelea vifaranga ,kama kawaida

👉Weka joto, vyombo vya maji, vyombo vya chakula

👉Hakikisha sana kama unatumia, mkaa madirisha yako yanakua yanaruhusu hewa kuingia , unaacha uwazi kidogo kuepusha baridi kuingia bandani

👉Vyanzo vya joto viwepo bandani walau Massa 24 kabla ya vifaranga kufika kuleta joto kwenye sakafu na randa

👉Tandika magazeti, au mifuko kwa siku 3-5 na ubadilishe kila yatakapo chafuka ( kilasiku)

👉Chakula na maji viwekwe masaa mawili kabla ya vifaranga kufika

👉Mita moja mraba vifaranga 40, eneo liongezeke kadri vifaranga watakao kua wanaongezeka

👉👈NB muda wa kufanya brooding unatofautiana, maeneo ya baridi wiki 3-4, maeneo ya joto wiki 1-2.

VIASHIRIA VYA HALI YA HEWA BANDANI

👉BARIDI IKIZIDI vifaranga wanakusanyika pamoja, au karibu na chanzo cha joto, suluhu ongeza joto

👉JOTO LIKIZIDI, viafaranga wanahema sana kwa kutanua mdomo, wanakaa pembezoni mwa brooder, wanaacha kula, wanakimbia vyanzo vya joto. Suluhu punguza chanzo cha joto

👉 Upepo mwingi vifaranga wanazunguka kwa makundi bandani, watakimbia eneo upepo unakoelekea kuja eneo upepo unapo ingilia, Kumbuka upepo unaoingia unakua na baridi

👉 Joto sahihi, Vifaranga hutawanyika vizuri bandani, na hula na kunywa maji, hivo ukuaji wao huwa wa kuwiana vizuri.

IMEANDALIWA NA
👈👉Greyson Kahise
Mtaalamu wa kuku
0769799728 0715894582

Jipatie kitabu changu cha FUGA KUKU KITAALAMU 10000 tu.