MAKALA JUU YA
CHANJO ZA KUKU WA AINA ZOTE.

Kuna aina tofauti za magonjwa kama MAGONJWA YA VIRUSI MAGONJWA YA BAKTERIA NA MAGONJWA YA KUPE/VIROBOTO/MINYOO.

MAGONJWA YA VIRUSI KWA KUKU NI KAMA

IBDauGUMBORO

MAREX

INFECTIOUS CORTYZA/MAFUA MAKALI

FOWL POX/NDUI

ILT ..INFECTIONS LARYNGOTRACHEITIS

NEWCASTLE/KIDELI

Magonjwa haya yasababishwayo na virusi HAYATIBIKI hivyo mfugaji ni vema ukawachanja kuku wako kwa moja ya mifumo ifuatayo....

 CHANJO KIPINDI TU KUKU AKIWA

AMETOTOLEWA DAY OLD CHICK//HATCHERY ACHANJWE

Chanjo ya Mareks kwa kuku wa mayai...(l(SASSO ..KLOIRER...PURE LAYERS....BREEDER

ISIPOKUA PURE BROILERS))

Chanjo ya IBD/Gumboro

Chanjo NEWCASTLE/KIDELI

 *MFUMO WA KWANZA*

SIKU YA KUMI CHANJO YA KIDELI/ND

SIKU YA 18 CHANJO YA GUMBORO/IBD

SIKU YA 28 CHANJO YA KIDELI/NEWCASTLE

SIKU YA 30 CHANJO YA NDUI/FOWL POX

KILA BAADA YA MIEZI MITATU AU WIKI 9 WAPE CHANJO YA KIDELI/NEWCASTLE HADI PALE UTAKAPO WATOA KUKU WAKO..

MFUMO WA PILI

SIKU YA SABA CHANJO YA KIDELI/NEWCASTLE

SIKU YA 14 CHANJO YA GUMBORO/IBD

SIKU YA 21 CHANJO YA NEWCASTLE//KIDELI

SIKU YA 30 CHANJO YA NDUI/FOWL POX

KILA BAADA YA MIEZI MITATI RUDIA CHANJO YA NEWCASTLE MPAKA UTAKAPO WATOA KUKU

NB+ Majina ya chanjo husika utajifunza kwa wauzaji wa madawa wanazijua hizo chanjo vizuri

VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHANJA KUKU

==Siku ya kuchanja kuku hakikisha kuku wametolewa maji asubuhi kabisa//uwanyime maji kwa Massaa 3au4

==Vyombo vyako vya kuwekea chanjo vioshwe vizuri kwa maji safi.

==Maji ya kuwekea chanjo yawe masafi na yachanganywe na Coper au chlorex blue ili kuondoa chlorine ya kwenye maji kufanya chanjo iwe na nguvu.

==Chanjo iliyotunzwa kwenye friji ichanganywe kwenye maji kutokana na uwingi wa kuku::Mara nyingi kopo moja la chanjo ni kwa kuku 500 dozi ndogo na 1000 dozi kubwa kwahio angalia unakuku wangapi alafu wachanganyie maji watakayo weza kumaliza.


==Wape maji yenye chanjo kwa muda wa saa1 hadi masaa2 alafu toa maji yenye chanjo.

==Dakika 5 baada ya kuweka chanjo angalia kama kuku wote//vifaranga wote wamekunywa maji yenye chanjo  kwa kutazama midomo yao itakua na rangi ya yale maji yenye copper.

==Kama kuna kifaranga hajanywa maji yachanjo mnyweshe kwa kijiko,,,au syrynge(bomba la sindano).

Chanjo ya ndui huchomwa kwa sindano kwenye bawa nivema umuite mtaalamu akuelekeze

BROILERS HAWACHANJWI FOWL POX/Ndui

HII NDIO MAKALA JUU YA RATIBA SAHIHI YA CHANJO

 IMEANDALIWA NA GREYSON KAHISEMTAALAMU WA UFUGAJI WA KUKU 0769799728 kwa maelezo na mawasiliano zaidi.