UOTESHAJI WA MAJANI HYDROPONICS FODDER

Hydroponics ni majani au mboga mboga zinazooteshwa kwa muda mfupi...hapa naongelea majani au nafaka za kulishia mifugo

HATUA ZA KUFUATA

Unachukua aina yoyote ya nafaka mfano. Mtama, mahindi au uwele

Unaosha nafaka utakayo amua kutumia kwa jiki kama inapatikana

Baada ya hapoo unayatoa kwenye maji uliyokuwa unasafisha hizoo nafaka

Unaloweka nafaka uliyoisafisha kwa maji safi kwa muda wa masaa 12

Baada ya masaa 12 nafaka yako itakuwa imeshapata maji ya kutosha

Unaziweka nafaka zako kwenye chombo ambacho kinapatikana sana sana wanatumia trey maalum za kuwekea ambazo zipo kama sahani au sinia

unazifunika kwa nylon yoyote lakini sana sana wengi wanatumia gazeti au nylon nyeusi

Unaziweka kwenye chumba ambacho hakipitishi mwanga kwa muda wa masaa 48

Baada ya masaa 48 ukienda kufunua utakuta nafaka uliyochagua imeota nyuzi nyuzi nyeupe

utatakiwa utoe trey za hiyo nafaka uliyochagua na kuweka sehemu iliyotengenezwa rasmi kama kichanja

 tray zina beba gram 200-500...na kuendelea inategemeana na ukubwa

Utatakiwa uwe unamwagilia maji kila maraa ziwe na unyevu

Baada ya siku nne kuanzia ile siku uliyoweka kwenye kichanja utatakiwa uwape kuku wako kwasababu itakuwa tayari

 Kwa ajili ya matumizi na baada ya siku saba unaweza kuwapa wanyama wengine kama sungura, ng'ombe, mbuzi, nguruwe

Majani haya huweza kupunguza kwa kiasi matumizi ya chakula pia huwa ni muhimu kwa kuongeza vitamin kwa kuku na kupelekea afya bora.

NB HAKIKISHA TREY ZAKO ZIMEOSHWA NA KUFANYIWA DISINFECTION/OSHA KWA MAJI YALIYO CHEMKA

Kuzuia Moulds na Fangasi

By KAHISE MTAALAMU WA KUKU NA SARAPIA

0769799728/0715894582